Mshambuliaji wa klabu ya Mtibwa Sugar, Jaffari Kibaya (Kati kati Pichani), akiwaongoza wenzake kushangilia bao alilofunga kwenye moja ya mchezo wa ligi kuu Tanzania bara
Akizungumza na Eatv Afisa mtendaji wa Mtibwa Sugar, Swabri Abdul amesema kutoutumia uwanja wa Manungu Complex msimu huu kumewapa changamoto kubwa kwani wachezaji wake hawajauzoea vyema uwanja wa CCM Gairo ambao hawautumii mara kwa mara katika mazoezi yao ya kilasiku.
Aidha Swabri amesema watajipanga vizuri kuhakikisha wanapata ushindi katika mchezo wao wa mwisho kesho dhidi ya maafande wa Ruvu shooting mchezo utakaopigwa katika dimba la CCM Gairo Mjini Morogoro.
Awali wakaguzi wa viwanja nchini waliufungia uwanja wa Manungu kutokana na kutokukidhi vigezo vya kanuni za viwanja na hatimaye timu ya mtibwa kuchagua kuutumia uwanja wa ccm Gaiiro kama uwanja wa nyumbani.
Wakatamiwa wa Mtibwa Sugar wenye alama 42 katika nafasi ya 15 watalazimika kushinda katika mechi yao ya mwisho huku wakiiombea Mwadui ambayo ipo nafasi ya 14 na alama zao 44 wapoteze ili wakwepe janga la kushuka daraa.
Ikumbukwe timu 4 zilizo chini ya msimamo wa VPL zitaporomoka daraja huku zilizo nafasi ya 15 na 16 zitacheza mechi za mtoano na vilabu kutoka daraja la kwanza ili kujua hatma ya kurejea msimu ujao wa ligi kuu.




