Saturday , 25th Jul , 2020

Mkurugenzi mstaafu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Hellen Kijo Bisimba amesema Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa alikuwa na mchango mkubwa katika kuiinua na kuboresha heshima kwenye sekta ya elimu.

Mkurugenzi mstaafu wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) Dkt. Hellen Kijo Bisimba

Amesema hayo leo Julai 25, 2020 katika mahojiano kwenye kipindi Maalum cha Maombolezo kinachoruka East Africa Television na East Africa Radio.

Ameongelea kwa kina mchango wa Marehemu Rais mstaafu Mkapa katika sekta mbalimbali katika kipindi cha utawala wake hadi umauti ulimpokuta Tarehe 24/07/2020.

“Mkapa alivyoingia alisimamia sana mambo yakuheshimu elimu watu kufuata mambo ya shule waende chuo wasome wawe na vyeti na sio mambo yakubabaisha”, amesema.

Aidha Dkt. Kijo Bisimba alifafanua kuwa katika kipindi Rais Mkapa anaingia madarakani watu walikuwa wanadharau sana elimu kwani waliiona kama ni kujipoteza muda ukizingatia kulikuwa na njia nyingi za kutafuta pesa kirahisi kwa wakati huo.

“Mimi mwaka huo wa 1995 ndo nilimaliza shahada yangu ya kwanza wakati huo  watu walikuwa wanadharau sana elimu hapo nyuma ukiwa unasoma watu wanakushangaa kwanini unapoteza muda kusoma'', amesema.

Zaidi tazama Video hapa