Saturday , 25th Jul , 2020

Klabu ya Paris Saint German ya imetwaa taji la Ufaransa( French Cup) kwa mara ya 13 baada ya kuifungwa Saint Etienne kwa bao 1- 0 kwenye mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia leo.

Mshambuliaji wa PSG, Neymar Jr akiwa na taji la French Cup walilolitwaa jana baada ya kuifunga Saint Etienne bao 1-0 alilofunga yeye mwenyewe.

Bao pekee la ushindi la PSG lilifungwa na mshambuliaji wake Neymar Junior dakika ya 14 ya mchezo na kuianzishia vyema mwendo wa ushindi matajiri hao wa Ufaransa ambao wanajiwinda na mchezo wa robo fainali wa ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Atalanta ya Italia.

Katika mchezo huo, Kylian Mbappe alishinda kuumaliza mchezo baada ya kupata majeraha kufuatia rafu mbaya aliyochezewa na nyota wa Saint Etienne Loic Parren ambaye alilimwa kadi nyekundu dakika ya 31 ya mchezo.

Mbappe ambaye msimu huu ameifungia PSG mabao 29 katika michezo 33, aliondolewa uwanjani huku akilia na mashaka makubwa ni kwamba huenda akaikosa mechi ya robo fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Atalanta itakayopigwa mapema mwezi wa nane.

Katika mchezo huo ambao ni wa kwanza wa mashindano nchini Ufaransa baada ya COVID-19, mashabiki takribani 5000 waliruhusiwa kuingia kwenye uwanja wenye uwezo wa kuchukua mashabiki 80000.