Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii nchini Tanzania, Dkt Kebwe Steven Kebwe.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Kebwe Steven Kabwe, amesema hayo leo katika mahojiano na East Africa Radio, juu ya jitihada za serikali katika kuhakikisha kuwa virusi vya ugonjwa huo haviingii nchini.
Kwa mujibu wa Dkt Kebwe, hivi sasa kuna vifaa vya kutosha kwa ajili ya kupima watu wote wanaowasili nchini kupitia katika mipaka na viwanja vya ndege, na kwamba idadi kubwa ya wahudumu wa afya wamepata mafunzo ya namna ya kutambua, kudhibiti kusambaa pamoja na kuhudumia mtu atakayebainika kuwa na ugonjwa wa Ebola.
Hata hivyo, waziri Kebwe amesema kupungua kwa maambukizi ya ugonjwa huo katika nchi za Afrika Magharini hakuwezi kuifanya Tanzania ibweteke na kulegeza hatua inazochukua sasa katika kukabiliana na ugonjwa huo.