Tuesday , 21st Jul , 2020

Ronaldo ni mnyama, Dzeko je tumwiteje?

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 50 katika ligi za Serie A, La Liga na Premier League wakati akipachika mabao mawili dhidi ya Lazio Jumatatu.

Cristiano Ronaldo na Edin Dzeko

Cristiano Ronaldo amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mabao 50 katika ligi za Serie A, La Liga na Premier League wakati akipachika mabao mawili dhidi ya Lazio Jumatatu.

Ushindi huo unaipeleka Juve kwenye hatua za mwishoni kuelekea ubingwa wa tisa mfululizo wa Serie A wakihitaji alama 4 tu kukamilisha kazi.

Ronaldo anaifukuzia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza wa Juve kuchukua kiatu cha dhahabu tangu Alessandro del Piero afanye hivyo msimu wa 2007-08, ambapo hadi sasa Mreno huyo na Ciro Immobile wa Lazio kila mmoja ana magoli 30.

Ronaldo amekuwa na wastani mzuri wa ufungaji kwa ligi zote tatu alizocheza, akifunga mabao 84 katika michezo 196 akiwa na Manchester United kwenye EPL

Pia alifunga mabao 311 katika michezo 292 akiwa na Real Madrid kwenye La Liga na mabao 51 katika michezo 61 akiwa na Juve kwenye Seria A hadi sasa.

Mabao 51 kwa Nahodha huyo wa Ureno ni mabao ya haraka kwenye karne hii kufungwa kwenye Serie A, kwa michezo 61.

Edin Džeko

Nikiandika kuhusu huyu mtu unarudisha mawazo yako kipindi kile kocha Roberto Mancini akisimama kwenye eneo lake la ukocha akimuelekeza mshambuliaji huyu nini cha kufanya uwanjani kwenye mechi za Manchester City msimu wa 2010/2011 hadi 2014/15.

Dzeko alifunga mabao 50 katika ligi tatu, akifunga mabao 50 kwenye mechi 130 za EPL akiwa na Manchester City kuanzaia msimu wa 2011-2016, Pia akifunga mabao 66 katika mechi 111 akiwa na Wolfsburg ya Bundesliga, Ujerumani kuanzia 2007-2011

Mbosnia huyo pia amefunga mabao 69 katika mechi 139 akiwa na AS Roma kwenye serie A hadi hivi sasa kuanzia 2015-2020.