Lionel Messi
Kwa mara ya kwanza tuzo za Ballon d'or hazitofanyika mwaka huu tangu zilipoanzishwa mwaka 1956 kutokana na janga la corona kuathiri shughuli za michezo mwaka huu.
Nyota wa Barcelona Lionel Messi alishinda tuzo hiyo mara ya sita mwaka uliopita, akimshinda Cristiano Ronaldo aliyeshinda mara tano.
Katika kipindi cha muongo mmoja nyota hao wawili wamekuwa wakibadilishana tuzo hiyo, ingawa mwaka 2018 ilichukuliwa na Luka Modric.
Ballon d'Or, inayotolewa na jalida la soka la Ufaransa, imekuwa kila mwaka ikitoa tuzo hiyo tangu Sir StanleyMatthews alipokuwa mshindi wa kwanza miaka 64 iliyopita.



