Saturday , 18th Jul , 2020

Klabu ya Singida United ambayo imeshaporomoka daraja, imeishangaza klabu ya Ruvu Shooting katika uwanja wake wa nyumbani wa mabatini kwa kuwachapa kwa mabao 2-0.

Kocha wa Singida United Ramadhani Nswanzulimo (Kulia), akimpa maelekezo kiungo Haruna Moshi (Kushoto) katika mmoja ya mchezo wa ligi kuu Tanzania Bara.

Mabao ya Singida United yalifungwa na Seiri Arigumaho dakika 13 na Ramadhani Hashimu dakika ya60.

Huo ni ushindi wa wa 4 kwa Singida United msimu huu, ingawa wanaendelea kusalia mkiani mwa ligi hiyo wakiwa na alama 18 ,huku kipigo kwa Ruvu Shooting kikiendelea kuwaacha katika nafasi ya 10 wakiwa na alama 41.

Mchezo mwingine ulipigwa katika uwanjwa wa Kaitaba ambapo Polisi Tanzania iliitandika Kagera Sugar kwa mabao 2-1, mabao ya Sixtus Sabilo dakika ya 45 kwa mkwaju wa penati, na Marcel Kaheza dakika ya 86 huku la wenyeji Kagera likiwa ni la kujifunga la Idy Mobby dakika ya 18 ya mchezo.

Ushindi wa Polisi Tanzania unawasogeza hadi nafasi ya 5 baada ya kufikisha alama 54 na kuishusha Coastal Union ambayo leo imetoka sare na Biashara kwa bao 1-1.

Katika mchezo uliopigwa huko Mara,Biashara ilipata bao lake kupitia Ramadhani Chombo huku Dany Lyanga akiisawazishia Coastal Union.

Matokeo mengine Namungo ilitoka sare ya bao 1-1 na Prisons wakati Ndanda ikichapwa na Mbeya City kwa bao 1-0, nayo Mtibwa Sugar ilipoteza kwa bao 1-0 dhidi ya KMC.

Mbeya City imejiondoa katika mstari wa kushuka daraja baada ya kufikisha alama 42 ikiwa katika nafasi ya 13,wakati kupoteza kwa Ndanda 16 ikiwa na alama 40.