Thursday , 16th Jul , 2020

MSN ni kifupi cha majina ya washambuliaji waliounda safu matata iliyojua kucheka na nyavu na kutikisa Duniani.

Washambuliaji Luis Suarez wa kwanza (Kushoto), Neymar Jr (Kati) na Lionel Messi (Kulia) katika moja ya mchezo wa La Liga wakishangilia pamoja.

 

 

M-Ilisimama badala ya Messi (Lionel),S-Ilisimama badala ya Suarez (Luis) na N-Ilisimama badala ya Neymar(Junior)

Mnamo msimu wa 2014/15,MSN ilijitambulisha ulimwenguni baada ya kufanya mabalaa kwa kuiwezesha Barca kutwaa Treble(Mataji Matatu ndani ya msimu) La Liga,Copa del Rey,na Champions League kupitia mchango wao wa kucheka na nyavu.

Upande wa pili wa shilingi,Real Madrid ilikua na safu yao iliyojulikana kama BBC,B-Ilisiama kwa Bale(Gareth),B-Nyingine ilisimama badala ya Bemzema(Karim), na C-Cristiano Ronaldo ambayo nayo ilikua safu matata ya ushambuliaji .

Battle yao kwa misimu mitatu ilikua kama ifuatavyo

Msimu wa 2014/15.

MSN Mechi 151,Mabao 122,Assists 55.

BBC-Mechi 148,Mabao 100, Assists 46.

Msimu wa 2015/16.

MSN-Mechi 151-Mabao 131-Assists 55.

BBC-Mechi 115,Mabao 98 Assits 34.

Msimu wa 2016/17.

MSN -Mechi 148,Mabao 111,Assists 51

BBC-Mechi 120,Mabao 70, Assists 22.

Ukifuatilia MSN ilikua moto kuliko BBC,ingawa BBC ilianza kujengeka kuanzia mwaka 2009,Ronaldo na Bemzema walisajiliwa wakati Bale alijiunga na Real mwaka 2013.

.MSN ilianza na jiwe lao Lionel Messi lililopandishwa 2006,Neymar akajiunga na Barca 2013,wakati tarehe na mwezi kama huu mwaka 2014,Luis Suarez alijiunga rasmi na kuunda utatu mtakatifu uliozinyanyasa safu nyingi za ulinzi Barani Ulaya.

Mnamo Julai 9 mwaka huu Suarez alifunga bao pekee na la ushindi la Barcelona dhidi ya Espanyol,na kufanya awe mchezaji wa tatu wa ufungaji bora wa muda wote wa klabu hiyo akifikisha mabao 185 katika mechi 278 akimpiku Ladislau Kubala mwenye mabao 184.

-Kinara ni Lionel Messi mwenye mabao 638

-Wa pili ni Cezar mwenye mabao 232.

Ikumbukwe MSN ilibomoka baada ya Neymar Jr kuondoka mwaka 2017 na kutua PSG,akiwaacha Suarez na Messi,wakati BBC ilibomoka mwaka 2018 kufuatia Cristiano Ronaldo kutimkia Juventus na kuwaacha Bale na Bemzema.