Thursday , 16th Jul , 2020

Kocha mkuu wa klabu ya Tottenham Hotspurs Jose Mourinho amemwagia sifa mshambuliaji wake Harry Kane kwa kufunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1 dhidi ya Newcastle United ambayo yanamfanya afikishe mabao 200 katika ngazi ya vilabu.

Kocha wa Tottenham Hotspurs (Kulia), akimpongeza mshambuliaji wake Harry Kane kwa kufikisha mabao 200 ngazi ya vilabu.

Kane raia wa England mwenye umri wa miaka 26 alifikisha magoli 201 katika mechi 350 alizocheza katika vilabu vya Milwal aliyoifungia mabao 9, Leyton alifunga mabao 5, Leicester City aliifungia bao 2 na Spurs kafunga mabao 185.

Mourinho amemtaja Kane kama mshambuliaji anayelijua goli na amekua bora katika maeneo ya hatari, ingawa aliandamwa na majeraha msimu huu lakini amempa muda mwingi wa kucheza ambao auanutumia vyema awapo kikosini.

Ushindi wa jana unaisogeza kwa ukaribu Tottenham kupata nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya kwa kuwa wamefikisha alama 55 na wapo nafasi ya 7 kwenye msimamo .

Pia ni ushindi wa kwanza kwa Jose katika uwanja wa ST James Park baada ya kujaribu mara 8 akiwa na vilabu tofauti nchini England.