Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Abdulrahman Kinana akiwa kwenye Mkutano Mkuu.
''Niwaombe wajumbe wa Mkutano Mkuu, tutakapopiga kura tumpe kura zote Mgombea wetu bila hata moja kuharibika ili apate faraja yetu na kisha twende nchi nzima kwa umoja kutafuta kura za Rais Magufuli, Wabunge na Madiwani'', amesema.
Aidha Kinana ameongeza kuwa ''Hakuna uchaguzi mwepesi kama huu na nina uhakika mgombea wetu Magufuli atapata kura mara nyingi zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2015 na wabunge watakuwa wengi na madiwani pia'' - Kinana
Kupitia Mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM jana Julai 10, 2020 Magufuli alimsamehe Kinana na kumwagiza Katibu Mkuu Dkt. Bashiru Ally amwalike kwenye mkutano Mkuu.
Tazama Video hapo chini


