Thursday , 2nd Jul , 2020

Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Emereck Aubameyang amekua mchezaji wa kwanza wa klabu hiyo kufunga mabao 50 kwa haraka zaidi katika ligi kuu ya Uingereza, akitumia mechi 79.

Mshambuliaji wa Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang

Aubameyang amefunga mabao mawili katika ushindi wa Arsenal wa mabao 4-0 dhidi ya Norwich City usiku wa Julai Mosi na kufikisha jumla ya mabao 19, sawa na Jarmie Vardy wa Leicester City ambao kwa pamoja wanaongoza katika mbio za kuwania kiatu cha mfungaji bora wa msimu.

Mabao mengine ya Arsenal yalifungwa na Granit Xhana na Cedric Soares, ambapo ushindi huo unawasogeza hadi nafasi ya 7 katika msimamo wakifikisha alama 46 na kufufua matumaini ya kumaliza kwenye nafasi nne za juu wakati huu mechi sita zikiwa zimesalia.

Matokeo mengine ni kwa upande wa Chelsea ambao wamepoteza dhidi ya West Ham United kwa mabao 3-2 na sasa kuendelea kuacha nafasi wazi kwa vilabu vya Manchester United na Wolves kuingia ndani ya nne bora.

Mabao ya Chelsea yalifungwa na Willian, huku ya West Ham United yakifungwa na Tomas Sousek, Michael Antonio na Andry Yarmolenko. Leicester City ilipoteza dhidi ya Everton kwa mabao 2-1,mabao ya The Tofees yalifungwa na Richarlison na Glfyi Sirguson huku la kufutia machozi kwa Liecester likifungwa na Kelchi Iheanacho.

Katika mechi 12 tangu kuanza kwa mwaka 2020, Leicester City imeshinda mechi tatu, sare nne na vipigo vitano na sasa wanahatarisha nafasi yao ya kufuzu kucheza ligi ya mabingwa ulaya msimu ujao.

Leicester City inashika nafasi ya tatu wakiwa na alama 55,chelsea ya tano ikiwa na alama 54 wakati Manchester United ipo nafasi ya tano na alama zao 52.