Wednesday , 1st Jul , 2020

kocha wa Yanga Lucy Eymael amesema hawezi kufanya kazi na mchezaji wa aina ya Benard Morrison kutokana na tabia zake za utovu wa nidhamu

Kocha mkuu wa Yanga Lucy Eymael (pichani)akiwa katika majukumu yake ya moja ya mchezo wa VPL uwanjani.

Kocha mkuu wa klabu ya soka ya Yanga,Lucy Eymael amesema amesema nyota wake Benard Morrison amebadilika sana kitabia tofauti na ilivyokua awali.

Eymael raia wa Ubelgiji amesema anashindwa kutambua kipi kinamsibu nyota huyo wa kimataifa wa ghana ingawa amefaja jitihada za kutosha kuzungumza nae lakini haoni mabadiliko ya tabia mbaya ya mchezaji huyo.

Kocha Eymael amesema aliamua kutomjumuisha katika kikosi kilichoivaa Kagera Sugar jana kwenye mchezo wa kombe la FA uliomalizika kwa ushindi kwa wanajangwani wa bao 2-1 kutokana na changamoto za kinidhamu anazoendelea kuzionyesha winga huyo.

Aisha kocha wa Yanga amesema kwa sasa anauachia uongozi wa klabu hiyo kuamua hatma ya Morrison ambaye tangu kuwasili kwake nchini ameonyesha kiwango kizuri kiasi cha kuteka hisia za mashabiki wa soka hususan wa Yanga.

Hivi karibuni Morrison alizua sintofahamu kutokana na kufanya mahojiano na chombo cha habari ambapo alionekana kukataa kuwa amesaini mkataba wa miaka miwili na Yanga,kwa madai hafurahishwi na mambo yanayoendelea ndani ya klabu.

Licha ya kusamehewa kwa kosa la kutosafiri na klabu katika michezo ya ligi kuu dhidi ya Mwadui na Jkt Tanzania katika mikoa ya Shinyanga na Dodoma,nyota huyo ameripotiwa kuleta taharuki katika kambi ya klabu ilipokua ikijiwinda na mchezo dhidi ya Kagera Sugar.