Sunday , 10th May , 2020

Naibu Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Juliana Shonza ameisifu show ya Friday Night Live inayoruka East Africa TV kila siku ya Ijumaa kuanzia 3:00 hadi 5:00 usiku kwa kusema, ni miongoni mwa vipindi anavyovipenda na kuvifuatilia.

Pichani ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Juliana Shonza

Akikizungumzia kipindi hicho kupitia post aliyoiweka kwenye ukurasa wake wa Instagram ameeleza kuwa, kama mlezi wa hii tasnia huwa vinamsaidia  kujua masuala mbalimbali yanayoendelea kwenye upande huo.

"Miongoni mwa vipindi vya burudani huwa napenda kuvifuatilia ni Friday Night Live (FNL) kile kinaendeshwa na kina T-bway360, kama mlezi wa hii tasnia huwa inanisaidia sana kujua masuala mbalimbali yanayoendelea upande huo, ili sisi kama viongozi wa wizara tuweze kuyafanyia kazi, Bwana weee show ya jana hawa vijana wetu pichani wanamitindo "model" Ben Breaker na Calisah kidogo wapigane kwa maneno tu, nawapongeza sana waandaaji kwa kutowakutanisha pamoja kwa hali niliyoiona sijui kama ngumi zingekosekana" ameandika 

"Kikubwa nilichokiona ni kila mtu anatafuta umbwamba kwa mwenziye, huyu anasema mimi nina tuzo kibao za kimataifa, huyu anasema wewe hata biashara huna tutajie unafanya biashara gani na hizo tuzo zimekusaidiaje na maneno mengine mengi kwa walioangalia wanayafahamu. Nachotaka kusema ni nini, tasnia hii ya modeling bado inakua japo tunao wanamitindo wengi wanaofanya vizuri kimataifa na wanapeperusha bendera ya nchi yetu vizuri mifano michache tu ni Flaviana matata, Ladivamillen na Herieth Paul ambao hata katika kitabu chetu cha bajeti ya wizara mwaka huu tumewatambua

"Bahati nzuri mimi nawafahamu nyote wawili vizuri, Calisah kuna kipindi ulileta barua wizarani ulichaguliwa kushiriki mashindano fulani ya mitindo nje ya Tanzania ,nachoweza kusema wote ni wana mitindo wazuri na mnapambania ndoto zenu, funzo kwa vijana tujifunze kuheshimiana bila kujali nani ni mkubwa nani ni mdogo, kikubwa tufikie malengo yetu, inawezekana kweli kati yenu mmoja ni mwamba lakini tujifunze kuheshimiana vijana wenzangu" ameongeza