
Gari la polisi lililoenda kumuokoa baada ya tukio hilo
Mzee huyo ametambulika kwa jina la William Makhanu, amewashtua wanakijiji wa eneo lake baada ya kufanya tukio hilo na nia ya kufanyiwa tambiko kwa kabila lao la Bukusu ni kumtakasa na kuzuia laana kwenye familia.
Akizungumza na waandishi wa habari mmoja wa wazee wa Bukusu Jared Barasa amesema "Kulingana na mila na desturi zetu ni makosa, sisi kama wazee tutalazimika kumchinja kondoo kumtakasa pamoja na mkwe wake".
Aidha mmoja wa watoto wake aitwaye Wanjala amesema mzee wao aligoma kufungua mlango hadi walipolazimika kuuvunja akihofia adhabu ya kuchapwa viboko 20.
"Tulimuamuru aondoke chumbani ila alikataa hadi tukalazimika kuuvunja mlango, kama wanawe tunahisi aibu kubwa kwa kuwa tuna wake na labda huenda amekuwa akiwatumia wote"
Chanzo Tuko News, Kenya