
Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, na Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Spika Ndugai ameyabainisha hayo leo Mei 2, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, na kuongeza kuwa agizo la Mbowe kwa Wabunge wake wamelipokea kwa mikono miwili, na kwamba amekuwa ni kiongozi wa kuamrisha tu na ndiyo maana wanachama wake wengi wanahama, na kuongeza kuwa janga la Corona ni la Dunia nzima na hakuna ambaye anapenda kuona watu wakifa.
"Sisi halitushangazi hawa wenzetu kila jambo lazima waweke upinzani hata kama ni janga, Wabunge ni timu moja hauwezi kuamrisha tu wachezaji wako kwamba tokeni bila kuzungumza na wenzako, Wabunge wa CHADEMA wana bahati mbaya sana kazi yao ni kuamrishwa tu kama watoto wa Primary vile na wanalalamika kimya kimya sana kwangu" amesema Spika Ndugai.
Aidha Spika Ndugai alizungumzia suala la kupokea ushauri wa Mbowe "Wala siko tayari tena, yeye aendelee tu na Methodology zake kwa sababu muda mfupi ujao tutamaliza Bunge kwa kuzingatia tatizo la Corona na toka tumeanza tumezingatia na tumebadilisha mambo mengi sana".