Monday , 27th Apr , 2020

Naibu Waziri wa TAMISEMI Mwita Waitara, amesema kuwa kifo cha Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Evod Mmanda, kimetokea alfajiri ya kuamkia leo Aprili 27, 2020, baada ya kuugua kwa siku mbili na kufariki ghafla.

Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda wakati wa uhai wake.

Waitara ameyabainisha hayo mapema asubuhi, wakati akizungumza na Supa Breakfast ya East Afrika Radio na kusema kuwa mpaka sasa wanawasiliana na familia yake ili kujua utaratibu utakuwaje na kisha taarifa rasmi itatolewa kwa wananchi.

"Sisi tumejulishwa na nimeongea na Mh Waziri na kuniambia kwamba marehemu aliugua kwa muda wa siku mbili kwahiyo kifo chake kimekuwa cha ghafla, ni mwenyeji wa Kilimanjaro sasa tutawasiliana na familia tuone utaratibu ukoje na mambo mengine tutakayopanga kama ofisi tutawajulisha, lakini ni kweli comrade Mmanda hatuko naye tena" amesema Waitara.

Evod Mmanda amefariki usiku wa kuamkia leo Aprili 27, 2020, katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara, Ligula.