
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.
Dkt Mabula amechukua nafasi ya Dkt Zainab Chaula, ambaye ameteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Mawasiliano, ambaye amechukua nafasi ya Dkt Maria Sasabo ambaye amestaafu.
Aidha Rais Magufuli amemteua Profesa Abel Makubi, kuwa Mganga Mkuu wa Serikali, akichukua nafasi ya Profesa Mohamed Bakari Kambi, ambaye amestaafu.
Uteuzi wa viongozi hao wote unaanza leo Aprili, 22, 2020.