
Mchekeshaji Mr Beneficial
Sasa Mchekeshaji Mr Beneficial ambaye yupo nchini Marekani kwa sasa ameeleza kuwa, yupo ndani kwa muda wa miezi miwili na nusu kwa sababu ya kujikinga na virusi vya ugonjwa huo.
Akizungumza na EATV & EA Radio Digital, msanii huyo wa vichekesho amesema Marekani kila kitu kimesimama, kazi zinazoendelea ni za muhimu kama kufunguliwa kwa Hospitali na maduka ya vyakula tena hufunguliwa kwa ratiba maalum.
"Kwa kipindi hiki mambo mengi yamesimama huku Marekani, kazi zinazoendelea ni za muhimu tu kama hospitalini na maduka ya chakula, tena shughuli wanazofanya ni chache na zina ratiba zake, pia kuna aina ambayo unatakiwa kwenda kuchukua unachohitaji" ameeleza.
"Hata shughuli zetu zilizotuleta za ku-shoot filamu na kuigiza na wasanii wa huku zimesimama hadi Corona iishe, mpaka sasa hivi mimi nina mwezi kama wa tatu au wapili na nusu sijatoka ndani" ameongeza.