Tuesday , 21st Apr , 2020

Kumekuwa na stori ambazo zinaendela zikiwahusisha wasanii wa BongoFleva TID na Lulu Diva, kwamba wapo kwenye mahusiano japo wenyewe wamekuwa wanakana suala hilo.

Kushoto ni TID, kulia Harmonize

Mmoja wa watu waliofanya waamini kwamba wawili hao wapo kwenye mahusiano, alikuwa ni Harmonize baada ya kupost video fupi ikiwaonesha wamejirekodi wimbo wake kisha akaandika  "Mahusiano ninayoyapenda kwa sasa, washaanza kufanana mapenzi ni matamu"

Kwa upande wa TID akizungumza na  EATV & EA Radio Digital, amesema Harmonize ni mtoto mdogo bado na hapaswi kujua yeye anachokifanya.

"Konde Boy ni kijana hakuna mfano naye, anaweza akasema chochote na siwezi ku-comment chochote lakini hapaswi kujua, japo alichokisema kinaleta maana ila siwezi kubishana na mawazo yake ila akumbuke kwangu yeye bado ni mtoto mdogo".

Mahojiano kamili tazama kwenye video hapa chini.