Tuesday , 14th Apr , 2020

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana, ambaye kwa sasa yuko mkoani Mara amesema amelazimika kuweka sanitizer nyumbani kwake kwa ajili ya kujikinga na Virusi vya Corona kwa wageni wanaokwenda kumsalimia, lakini baadhi ya majirani zake wanamuona anajidai.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana.

Kamanda Shana amesema hayo leo Aprili 14, 2020, wakati wa mahojiano maalum na EATV& EA Radio Digital.

"Mimi nyumbani kwangu kwakweli nimeweka sanitizer za kutosha hata wageni wanokuja lazima wanawe mikono, japokuwa huku kijijini wanaona kama vile ni kujidaidai na matawi ya juu, wanasema ni mambo ya kizungu" amesema Kamanda Shana.

Kamanda Shana yupo mkoani Mara kwa ajili ya likizo.