Monday , 16th Mar , 2020

Tanzania kwa mara ya kwanza imethibitisha uwepo wa mgonjwa wa homa kali inayosababishwa na Virusi vya Corona.

Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.

Taarifa hiyo imetolewa leo Machi 16, 2020, na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu na kusema kuwa mtu huyo ni mwanamke aliyekuwa akitokea nchini Ubelgiji.

"Machi 15 tulipokea msafiri Mtanzania mwanamke (46),akitokea Ubelgiji kupitia Uwanja wa Ndege wa KIA, vipimo vya awali vilionesha hana homa, baadaye alianza kujisikia vibaya na kwenda Hospitali ya Mount Meru na vipimo vya maabara vimethibitisha kuwa mtu huyu ana maambukizi ya ugonjwa wa COVID-19" amesema Waziri Ummy