Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe.
Mbowe ameyabainisha hayo leo Machi 16, 2020, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari katika Ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, Ufipa jijini Dar es Salaam.
"Kuanzia April 4, hatutasubiri kibali cha Magufuli wala mtu yeyote, nawatangazia viongozi wote wa CHADEMA nchi nzima, kuanzia Majimbo, Kanda, Kata, Vijiji na Mitaa kufanya mikutano ya hadhara kwa utaratibu uliopo kisheria tukidai vitu viwili, kwanza ni kudai tume huru na pili ni maandalizi ya Uchaguzi Mkuu" amesema Mbowe.
Aidha Mbowe ameonesha kusikitishwa na vitendo vilivyofanya na Askari Magereza baada ya kuwajeruhi vibaya Wabunge halima Mdee, Ester Bulaya na Jesca Kishoa







