Monday , 16th Mar , 2020

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, amesema kuwa kitendo cha Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa kusema kuwa kina Mdee walienda kuvamia Magereza na kutaka kumtoa Mbowe kwa nguvu ni uongo ambao hata shetani anaweza kuja kujifunza.

Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema.

Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, Lema amesema kuwa kutokana na hayo yote zipo hatua ambazo kama chama wamepanga kuzichukua ili kuhakikisha mateso kama hayo ndani ya chama chao yanakwisha.

"Niliposikia kauli ya Mambosasa imenishangaza, nafikiri sasa shetani anaweza kuja kujifunza tuition ya uongo duniani, kitendo walichofanyiwa akina Halima, Ester na Jesca ilibidi wanawake wote nchi nzima wapige kelele" amesema Lema.

Wabunge Ester Bulaya, Halima Mdee na Jesca Kishoa, wamelazwa katika Hospitali ya Agakhan, kufuatia majeraha waliyoyapata kwa kile kilichoelezwa kuwa walipigwa na Polisi.