Msanii Harmonize
Akiongea na eNewz ya East Africa Television, Harmonize amesema kati ya hizo 18 ngoma 15 zote ni mpya huku zile tatu zikiwa ni Uno, Hainishtui na Hujanikomoa.
'Unajua nimejitahidi sana kuhakikisha ngoma nyingi kwenye Afro East zinakuwa mpya kwahiyo watu watakaokuja na wale ambao hawatafika watafurahia albam hii wakinunua', amesema.
Kuhusu wale atakaohudhuria uzinduzi huo unaofanyika Mlimani City Harmonize amesema Mama yake, Baba yake na mke wake huenda wakawepo kama itampendeza Mungu maana usiku huo atakuwa pia anasherehekea Birthday yake na ameahidi itamkuta jukwaani akitumbuiza.
Zaidi Tazama Video hapo chini
