Tuesday , 10th Mar , 2020

Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha, limekanusha taarifa za uvumi zilizokuwa zimeenea katika mitandao mbalimbali ya kijamii, zikieleza kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai Lengai Ole Sabaya, alimjeruhi mtu kwa kumpiga risasi kwenye kumbi za starehe.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana

Akizungumza leo Machi 10, 2020, na EATV&EA Radio Digital, Kamanda wa Polisi mkoani humo Jonathan Shana, amesema kuwa ndani ya Mkoa wake, hakuna tukio la namna hilo na kwamba Sabaya ni kiongozi muadilifu.

"Kwa kawaida mtu akipigwa risasi ama kujeruhiwa anapaswa kutoa taarifa kituo chha Polisi, hata mimi baada ya kuona hizo taarifa zinasambaa, nimetafuta katika vituo vyangu vyote hakuna, kwahiyo sisi hatuna taarifa kama hiyo kwenye vituo vyetu" amesema Kamanda Shanna.