Mchekeshaji Anko Zumo
Akieleza sababu ya kutoa talaka hizo kwa wake zake waliopita, Anko Zumo amesema hajawahi kufumaniwa, kufumania wala kusaliti ila ni matatizo binafsi waliyokuwa nayo wake zake hao na kwenye masuala hayo.
"Sijawahi kufumania wala kufumaniwa, maana hayo ndiyo mambo makubwa ambayo yanafanya watu waachane, mke wangu wa kwanza nilimpa talaka kwa sababu hakuijua ndoa vizuri, umri, maneno ugomvi hadi tukaachana" amesema Anko Zumo.
Pia ameendelea kusema "Mke wa pili nilimpa talaka kwa sababu nilikurupuka, maana tulikaa mwaka mmoja kisha tukaachana, kulikuwa na migogoro mingi hadi nikampa talaka tatu, nimeshakuwa mzoefu wa haya mambo hata Dr Mwaka hataniweza kwenye kuachana achana maana nipo kwenye ndoa kwa miaka 13" ameongeza.

