Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema.
Akizungumza na EATV&EA Radio Digital, leo Machi 3, 2020, Kamanda wa Polisi Mkoani humo Sweetbert Njewike, amesema kuwa bado wanaendelea kumshikilia na uchunguzi ukikamilika watamfikisha mahakamani.
"Tumemkamata baada ya kutoa taarifa zisizo sahihi, kwahiyo tunamhoji na baada ya hapo tutampeleka mahakamani" amesema Kamanda Njewike.
Jana usiku Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kanda ya Kaskazini, Aman Golugwa, alitoa taarifa za Mbunge Lema kusafirishwa na Polisi kutoka Arusha hadi Singida kwa ajili ya mahojiano.
