Tuesday , 3rd Mar , 2020

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya linawashikilia watuhumiwa 11 kwa madai ya kufanya uhalifu kwa njia ya mtandao kwa kutumia majina ya watu maarufu ikiwemo la Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe Jokate Mwegelo, wasanii Wema Sepetu, Aunt Ezekel, Jackline Wolper na Kajala Masanja kujipatia fedha.

Katika picha ni Wema Sepetu, Jokate Mwegelo na Jackline Wolper.

Hayo yamebainishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya,Ulrich Matei, wakati akizungumza na waandishi wa habari ambapo amesema, Jeshi la Polisi Mkoa kwa kushirikiana na kitengo cha upelelezi, waliwabaini watuhumiwa hao tangu Februari 22 mwaka huu.

Aidha Kamanda Matei ameeleza kuwa watuhumiwa hao ambao miongoni mwao,wawili wana sajili laini za simu, walikuwa wakiwapigia watu simu na kuwafahamisha kuwa, wao wametumwa na Jokate Mwegelo ili kuwapatia wananchi mikopo nafuu pamoja na ajira.