Tuesday , 3rd Mar , 2020

Gwiji wa zamani wa soka katika klabu ya Simba na nchi ya Tanzania, Damian Mrisho Kimti amefariki dunia Machi 2, 2020 Jijini Dar es Salaam.

Damian Mrisho Kimti ( Waliosimama, wa saba kutoka kulia )

Kimti alitamba na klabu ya Simba katika miaka ya 90, ambapo pamoja na mambo mengi aliisaidia kalbu hiyo kucheza fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati mwaka 1992.

Pia gwiji huyo alikuwepo katika kikosi kilichocheza fainali ya Kombe la CAF mwaka 1993 dhidi ya Stella Abidjan.

Klabu ya Simba imetoa taarifa rasmi ya kuelezea masikitiko yake kufuatia kifo cha gwiji huyo. Taratibu za mazishi zinatarajiwa kutolewa na wanafamilia na mwili upo Mbezi - Kimara, ambako alikuwa  aliishi wakati wa uhai wake.