
Picha ya mahali ambapo mwanafunzi huyo amejirusha
Naibu wa Jeshi la Polisi wa Mji wa Nakuru Daniel Kitavi, amesema mwanafunzi huyo amefariki wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya Thika Level V, ambapo alikimbizwa baada ya kujirusha kutoka ghorofani na kwamba aliumia zaidi maeneo ya kichwani.
Aidha wanafunzi wenzake walidai kwamba, mwenzao huyo alikuwa anajitishia kujitoa uhai kwa sababu ya matatizo yake binafsi.
Chanzo : Citizen Digital