Kutoka kushoto pichani ni Mwana Fa, Billnass na Maua Sama
Akizungumza kwenye show ya eNewz inayoruka kupitia East Africa TV kila siku za Jumatatu hadi Ijumaa kuanzia 12:00 mpaka 12:30 jioni, Mwana Fa amesema ameshawasaidia wasanii wengine kama Maua Sama na Billnass hadi pakachimbika kwa sababu haikuwa rahisi.
"Nimemshika mkono Billnass pia kwa hiyo siwezi kusaidia wasanii wote kwa wakati mmoja hiyo ni kazi kubwa sana hata kwa Maua Sama penyewe pamechimbika kwelikweli, sisemi kama nimefunga milango, ila kama nafasi ikitokea nikiona kuna uwezekano wa mimi kufanya hivyo nitaendelea kutoa sapoti" ameeleza Mwana FA.
Mengine zaidi aliyozungumza tazama zaidi kwenye video hapo chini.
