
Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo
Akizungumza na watumishi wakiwemo viongozi mbalimbali wa Halmashauri ya Kisarawe Waziri Jafo, amesema Serikali imefanikiwa kupeleka huduma za kijamii wilayani humo hivyo ni wazi kuwa ipo haja ya kuboresha miundombinu ya makazi.
Aidha Mkurugenzi wa Halmashauri Mussa Gama amesema tayari ameshamuandikia barua Mkurugenzi wa TBA Makao Makuu na anachosubiri ni utekelezaji wa agizo hilo.
Kwa upande wake baadhi ya wakazi wa Kisarawe wamefurahia hatua hiyo na kusema itasaidia kuboresha Mji huo.
#HABARI Waziri wa TAMISEMI, Selemani Jafo amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kisarawe kuiandikia barua TBA ya kuitaka kuvunja majengo chakavu na kujenga majengo mapya yatakayolingana na mabadiliko ya ukuaji wa Mji huo. pic.twitter.com/YBlIeKcqlP
— East Africa Radio (@earadiofm) January 1, 2020