
Pichani ni Faru Fausta aliyefariki Dunia.
Robert Fyumanga ni daktari wa Wanyamapori, amesema kuwa kuta za moyo wa Faru Fausta, zilikuwa nyembamba sana hali iliyopelekea damu ishindwe kupita kwa ufasaha.
"Kuta za Moyo wake zimekuwa ni nyembamba sana hivyo kushindwa kusukuma damu ya kutosha mwilini, kwahiyo alikosa nguvu na kuanguka" amesema Dkt Fyumanga.
Faru jike mweusi ambaye alipewa jina la Fausta, ambaye pia ndiye Faru mzee kuliko wote duniani, alifariki dunia siku ya jana ya Disemba 28, 2019, katika eneo alilokuwa akihifadhiwa kutokana na maradhi ya uzee.