
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara, Blasius Chatanda.
Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi mkoani humo, Blasius Chatanda, amesema kuwa wao wamejipanga ipasavyo ikiwemo kuweka ulinzi wa kutosha kuanzia majini hadi nchi kavu.
"Tumejipanga ipasavyo kwa kufanya doria kuanzia majini ili kuzuia wale wanaodhani wanaweza kuingia Mtwara, kuja kufanya uhalifu kupitia majini kwa maana ya baharini hadi mto Ruvuma, hapa mwanzo unapoanzia hadi kule mwisho upande wa nchi jirani ya Msumbiji" amesema Kamanda Chatanda.
Aidha Kamanda Chatanda akatoa rai kwa wazazi na walezi, wasiwaachie watoto kwenda fukweni bila ya kuwa na waangalizi.