
Kaka wa Tito Magoti, Edwin Magoti.
Hayo ameyabainisha leo Disemba 21, 2019, wakati akizungumza na Waandishi wa Habari na kutoa rai kwa vyombo vya ulinzi na usalama na Serikali kwa ujumla ilichukulie suala hilo kwa uzito ili wajue hatma yao.
"Kama familia tumeendelea kusikitishwa na hakuna amani kabisa, licha ya Polisi kusema wako naye lakini hatujui yuko wapi, nadhani njia iliyotumika kumkamata sio sahihi hata kama angekuwa ni mhalifu, kuna taratibu za kufuata, niomba Serikali ilichukulie suala kwa uzito wake, tujue nini kinafanyika na tujue taratibu zingine za kumtafutia dhamana ziweze kufanyika" amesema Edwin.
Tito Magoti alikamatwa jana Disemba 20, 2019, majira ya saa 4:00 asubuhi maeneo ya Mwenge, na baadaye Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa, alithibitisha kumshikilia kwa sababu za kiupelelezi ambazo hazitoweza kuwekwa hadharani.