
Mbunge wa Kibamba na Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika.
Mnyika ametangazwa usiku wa kuamkia leo Disemba 20, 2019, ambapo amechukua nafasi ya ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Vicent Mashinji.
Aidha Baraza hilo pia limeridhia uteuzi wa Salum Mwalim, kuendelea na nafasi yake ileile ya Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, ambapo pia limemteua Singo Kigaila, kuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara na John Heche kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu.
Usiku wa kuamkia jana Disemba 19, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kilimchagua Freeman Mbowe kuwa Mwenyekiti wa Chama hicho, Tundu Lissu kuwa Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara na Said Issa Mohammed, kuwa Makamu Mwenyekiti Zanzibar.