
Mmoja wa majeruhi
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa Bukoba Dk. Mussa Sweya amekiri kupokea maiti mbili na majeruhi watano, na kuwa majeruhi wawili wametibiwa na kuruhusiwa kutokana na kuwa na majeraha madogo.
Pia amesema kuwa majeruhi watatu wamelazwa, na mmoja amefanyiwa upasuaji mkubwa, kutokana na kuathirika zaidi na majeraha hayo ya visu.
Mzazi wa mmoja wa majeruhi Athuman Mujuni ameeleza alivyopata taarifa za mtoto wake kuchomwa visu na kumkuta utumbo ukiwa nje.
Akizungumza kwa njia ya simu kamanda wa polisi mkoani Kagera, Revocatus Malimi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa wameanza uchunguzi ili kubaini chanzo.