Thursday , 31st Oct , 2019

Kocha wa timu ya Kagera Sugar Meck Mexime, amesema walikuwa na presha kubwa ya kushinda nyumbani na hali hiyo ilikuwa inafanya kila mchezo unakuwa mgumu kwao.

Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime

Mexime amekiri hilo baada ya ushindi waliopata jana Oktoba 31, 2019 dhidi ya Namungo FC wa magoli 2-0, na kuwafanya sasa wapate ushindi wa kwanza kwenye uwanja wa nyumbani.

'Mechi ya jana ilikuwa ngumu kwetu maana tulikuwa na presha ya kushinda katika uwanja wa nyumbani, angalau tumefanikisha hilo sasa tutaendelea kufanya vizuri', amesema Mexime.

Aidha kwa upande wake kocha wa Namungo FC iliyopanda daraja msimu huu, Hitimana Thierry, amedai kuwa majeruhi wengi walionao ndio sababu ya kupoteza mechi ya nne ugenini.

Wakati huo Mashabiki wa timu ya Kagera Sugar wamewaomba wachezaji wa timu hiyo kuongeza nguvu na kujituma zaidi ili kurejesha imani kwa Wanakagera, iliyokuwa imepotea kutokana na timu yao kunusurika kushuka daraja katika msimu uliopita, na kufungwa mechi mbili mfululizo katika uwanja wa nyumbani katika msimu huu.