uwanja wa Ndege wa Msalato na ujenzi wa barabara za mzunguko.
Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) Dkt. Akinwumi Adesina, ameyasema hayo katika Ofisi za Makao Makuu ya Benki hiyo yaliyopo Abijdan Nchini Ivory Coast, wakati wa mazungumzo yake na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba John Kabudi,
Amesema Benki hiyo tayari imeshaidhinisha kiasi cha Dola za Marekani milioni 180, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko jijini Dodoma, na kwamba kiasi kingine cha Dola za Marekani milioni 275 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Msalato.
Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Prof. Palamagamba Kabudi, ameishukuru Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa ushirikiano inayoutoa kwa Tanzania, hususani katika utekelezaji wa miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambayo kimsingi yalikuwa ni maono ya Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa nia ya kuiwezesha Tanzania kujitegemea kiuchumi na hatimae Bara zima la Afrika.



