Kocha wa Yanga na wachezaji wake
Yanga wanajiandaa na mchezo wao wa awali dhidi ya Pyramids FC, kutafuta nafasi ya kufuzu hatua ya makundi ya kombe la Shirikisho, utakaochezwa kesho kutwa Jumapili kwenye uwanja wa CCM Kirumba, Jijini Mwanza.
Akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kumaliza mazoezi ya leo, kocha huyo amesema kuwa, amefanya hivyo ili kutoa motisha kwa wachezaji wake na kuwapa nguvu ya kupamba ili waweze kuipata pesa hiyo.
Aidha, Zahera akazungumzia namna ambavyo amewapanga washambuliaji wake katika mchezo huo na kuwapa mbinu za namna gani wanatakiwa kushambulia.
Yanga inatarajia kushuka dimbani dhidi ya matajiri hao wa Misri Jumapili hii, baada ya kuondolewa na Zesco United katika hatua ya pili ya Klabu Bingwa Afrika, huku Pyramids wenyewe wakifanikiwa kuiondoa CR Belouzdad ya Algeria kwa uwiano wa mabao 2-1.



