Saturday , 28th Sep , 2019

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohammed Dewji ametembelea uwanja mpya wa mazoezi wa klabu hiyo unaojengwa eneo la Bunju Jijini Dar es Salaam.

Mo Dewji akiwa katika ukaguzi wa uwanja

Klabu hiyo iko katika mkakati wa ujenzi wa kituo chake ambacho kitakuwa na viwanja vya mazoezi, hosteli za wachezaji pamoja na 'gym', ambapo katika hatua ya kwanza ikianza na ujenzi wa viwanja viwili.

Akizungumza alipotembelea viwanja hivyo, Mo amesema kuwa hivi karibuni viwanja hivyo vitakamilika pamoja na vyumba vyake vya kubadilisha nguo.

Klabu ya Simba ipo kanda ya ziwa ikiendelea na mfululizo wa mechi za Ligi Kuu Tanzania Bara, ambapo katika mchezo wa mwisho dhidi ya Kagera Sugar iliibuka na ushindi wa mabao 3-0, mchezo uliopigwa Septemba 26, 2019 katika uwanja wa Kaitaba.