Monday , 23rd Sep , 2019

Mwili wa aliyekua Rubani wa ndege ndogo ya kampuni ya Auric Air , Nelson Mabeyo ambaye ni mtoto wa Mkuu wa Majeshi Nchini Jenerali Venance Mabeyo, umesafirishwa jioni ya leo kwa helkopta ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania ( JWTZ) kutoka Seronera (Serengeti) kuelekea Dar es Salaam.

Harakati za kusafirisha mwili.

Nelson alipoteza maisha katika ajali ya ndege ilitokea mapema asubuhi ya leo, ambapo ndege hiyo aina ya (Cessna 208B Caravan)ilianguka katika hifadhi ya Taifa ya Serengeti ikielekea Arusha.

Watu wawili waliokuwa kwenye ndege hiyo wamepoteza maisha, ambapo mmoja wapo ni Nelson Mabeyo ambaye alikuwa rubani. Aidha mwili wa rubani mwingine ambaye ni mwanafunzi, Nelson Orutu umesafirishwa hadi Jijini Arusha kwa taratibu za mazishi.

Rubani Nelson Mabeyo alihitimu kozi ya Urubani huko Florida Flyers Flight Academy nchini Marekani mwezi Februari 2017.