Saturday , 21st Sep , 2019

Timu ya taifa ya Tanzania kwa wachezaji wa ndani, ambayo inajiandaa na mchezo wa kufuzu michuano ya CHAN, dhidi ya Sudan, inaendeelea na mazoezi na kocha msaidizi Suleiman Matola amesema kambi ipo katika hali nzuri.

Wachezaji wa timu ya taifa wakiwa kwenye mezoezi

Matola ameeleza kuwa wachezaji wote 25 wapo vizuri na wametimiza program zote za mazoezi kilichobaki ni wao kufanyia kazi maelekezo wakiwa uwanjani.

'Tumefanya vikao na mchezaji mmoja mmoja baadaye wawili mpaka watatu, lengo likiwa ni kufanya vizuri na wao wamesema wana  hamu ya kutumia vizuri uwanja wa nyumbani', amesema Matola.

Tanzania inacheza mchezo wa kwanza na Sudan kesho Jumapili Septemba 21, 2019, kabla ya kucheza mchezo wa marudiano huko Sudan na kama watashinda kwenye matokeo ya jumla watafuzu CHAN 2020 itakayofanyika nchini Cameroon.