Miongoni mwa wawakilishi waliozungumza, kulia ni timu ya Mchenga
Kwenye ziara yao katika studio ya East Africa Radio leo, wawakilishi mbalimbali wa timu hiyo wameendelea kutambiana, ikiwa zimebaki siku mbili kabla ya kivumbi cha hatua ya 16 bora kufanyika katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay, Dar es Salaam.
Baadhi ya wawakilishi hao ambao wamezungumza leo ni nahodha wa mabingwa watetezi wa michuano hiyo msimu uliopita Mchenga Bball Stars ambaye ni Mudi alikuwa studio katika kipindi cha East Africa Breakfast pamoja na mwakilishi wa wapinzani wao Temeke Heroes kama inavyoonekana hapa chini.
"Acha waseme lakini kama ni noma kweli, msimu huu tunaleta burudani nyingine. Kikosi changu hakijabomoka bali kimeimarika, watu wetu tunawataka wawahi Jumamosi pale Don Bosco" - Mudi, mwakilishi wa Mchenga Bball Stars#EastAfricaBreakfast#SpriteBballKings#NomaKweli pic.twitter.com/4s4gYhQyQR
— East Africa Radio (@earadiofm) September 4, 2019
"Mchenga ni ya nchi nzima, vijana wangu wanatoka mikoani, tunasajili watu makini na ndio maana tunafanya vizuri na kuhakikisha hilo, msimu huu tumesajili hadi timu ya U-16" - Mudi, mwakilishi wa Mchenga Bball Stars#EastAfricaBreakfast#SpriteBballKings#NomaKweli pic.twitter.com/csSLeBznVc
— East Africa Radio (@earadiofm) September 4, 2019
Kwa upande wa mwakilishi wa Temeke Heroes aliyejitambulisha kwa jina la Tonge Masta akamjibu Mudi ambapo amesem,
"Mudi ni mwalimu wangu lakini sasa hivi niko katika chama la ushindi. Watu watarajie burudani nzuri ndani ya mchezo na nje ya mchezo, kwa sababu mimi pia ni mwana Hip Hop" - Tonge Masta, mwakilishi wa Temeke Heroes#EastAfricaBreakfast#SpriteBballKings#NomaKweli pic.twitter.com/cT8CmndhhK
— East Africa Radio (@earadiofm) September 4, 2019
"Hatua kama hizi kujipanga ni lazima hasa ukizingatia tunakutana na mabingwa watetezi Mchenga. Na sisi tumejiandaa, tunapiga mazoezi ya kufa mtu, hatuwezi kueleza sana tutakutana uwanjani"- Tonge Masta, mwakilishi wa Temeke Heroes#EastAfricaBreakfast#SpriteBballKings#NomaKweli
— East Africa Radio (@earadiofm) September 4, 2019
Aidha, mwakilishi wa Wagalatia ambaye alifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Supa Mix leo, alijigamba kuwa wako vizuri kuelekea mchezo wao wa Jumapili, Septemba 8 dhidi ya KG Dallas, amesema,
"Sisi Wagalatia tulijisajili wachezaji 9 lakini kwenye mtoano tulikuja 6 tu na tukacheza mchezo tukafuzu. Tumejiandaa vya kutosha sana" - Mwakilishi wa Wagalatia.#Supamix#SpriteBballKings#NomaKweli pic.twitter.com/Yb6uEY9svP
— East Africa Radio (@earadiofm) September 4, 2019
"Wachezaji wengi wa timu yetu tumetoka timu ya Chui inayomilikiwa na jeshi, tunazitaka milioni 10 ndio maana tukashinda kwenye mtoano tukiwa 6 tu. Tutaleta watu wetu kwenye 16 bora wanaojua kushangilia kiaskari" - Mwakilishi wa Wagalatia.#Supamix#SpriteBballKings#NomaKweli pic.twitter.com/p9hCj8B4JK
— East Africa Radio (@earadiofm) September 4, 2019
Ratiba nzima ya michezo ya hatua ya 16 bora wikiendi hii ni kama inavyoonekana hapa chini.