Wednesday , 10th Sep , 2014

Msanii Willy Paul, wa nchini Kenya amejikuta matatani hasa baada ya kufunguliwa mashtaka mahakamani kwa tuhuma za kuvunja sheria ya hakimiliki.

msanii wa muziki nchini Kenya Willy Paul

Willy Paul anatuhumiwa na msanii Elijah Prince kwa kuiba wimbo wake na kutumia sehemu ya kazi hii kutengenezea wimbo wake ambao unakwenda kwa jina 'Tamtam' bila idhini yoyote.

Nyaraka za mashtaka haya tayari zimekwishaonekana na shauri hili huenda likamtikisa kabisa msanii Willy Paul kisanaa endapo atapatikana na hatia.