Sunday , 25th Aug , 2019

Baadhi ya wananchi wa Kata ya Bagara, Wilaya ya Babati mkoani Manyara wamemuomba Waziri wa Maji, Prof. Makambe Mbarawa, kuwapelekea maji yaliyosalama kutokana na maji ya sasa wanayotumia si salama na yamekuwa yakiwasababishia magonjwa kila siku.

Kwa mujibu wa wananchi, maji ambayo wamekuwa wakiyatumia wamekuwa wakiyatilia shaka, kutokana kubadilika rangi mara baada yakuyachemshwa kwa kile walichokieleza maji hayo yanakuwa na rangi ya maziwa pindi wakiyachemsha.

Wakizungumza kwenye mkutano wa hadhara, katika muendelezo wa ziara ya kikazi ya Waziri Mbarawa, wamesema wamechoka kunyw amaji machafu kiula siku, huku maji yao yakionekana kuwa na gharama kubwa zaidi.

Akijibu malalamiko hayo, Waziri wa Maji Makame Mbarawa amewaomba wananchi hao kuwa wavumilivu, na kuwaahidi suala hilo atalipelekea kwa wataalamu wa maji ili  lisijirudie.

"Naomba sana ndugu zangu, muwe wavumilivu na [ia mniamini ili niweze kutatua matatizo yenu ya maji kwa umakini, na ufasaha, natambua na najua changamoto mnazopata kuhusu maji." amesema Mbarawa