Akizungumza na EATV & Radio Digital, Bugaywa amesema foleni ya Mbezi haiwezi kwenda kwa matakwa ya mtu binafsi kwa sababu njia ni moja na inatumiwa na magari ya kawaida na mabasi, hivyo hakuna muujiza wa kuyasogeza ili yawahi kuchukua abiria.
''Mbezi huwezi ukategemea mipango yako kwa sababu ile ni foleni na kuna wakati magari yanakata kabisa, hali ya barabara ndio inatafsiri aina ya huduma zitakayoendelea. Mbezi ni eneo ambalo barabara inatumiwa na magari mengine kwahiyo mfumo wa barabara zingine zitakavokuwa", amesema Buganywa.
"Mfumo utakavyokuwa kama kuna foleni lazima tu magari yatakwama kwenye foleni na hakuna muujiza wa kuyasogeza hapo na hata abiria wanajua na tumekuwa tukiwaelewesha katika hilo'', ameongeza.
Hatua ya kuutafuta uongozi wa DART, imekuja baada ya kushuhudia hali ya foleni ya watu katika eneo hilo, walioonekana kukaa kwa muda mrefu bila gari kutokea.