Kidoa
Akiongea kwenye Friday Night Live ya East Africa Television, Kidoa amesema mwanaume huyo alikuwa anajulikana kwao na alishatoa posa japo hawakuoana.
''Ngoja leo niseme ukweli, nimewahi kuishi na mwanaume lakini alikuwa mkristo na mimi ni muislam hivyo familia yangu haikunielewa japo alishatoa mpaka mahari'', - Kidoa.
Mrembo huyo ambaye amewahi kuingia kwenye mgogoro wa kukataa kuitwa Kidoa wa Akadumba, amesema kwa mwanaume huyo alikuwa anapata kila kitu ikiwemo safari za Dubai, China pamoja na kubadilishiwa magari kitu ambacho familia ya mwanaume huyo ilikuwa haipendi.