
Waziri ambaye ni msanii wa kujitegemea ameongea na eNewz kuwa kazi hiyo nzima yenye miondoko ya Afro Pop inatarajiwa kuwa tayari wiki ijayo ikiwa imabatizwa jina la 'Maneno Madogo Madogo' ambayo imefanyiwa MJ Records chini ya mkono wa Marco Chali.
Aidha, Waziri ambaye amewahi toa video aliyoshirikiana na msanii Chege iitwayo 'Tuli' ameongezea kuwa tayari kuna kolabo ambayo amefanya na msanii Chiby Dayo ambaye ni swahiba wake walioshiriki katika shindano hilo huku kazi nyingine nyingi zifuatiwa za kuwashirikisha wasanii wengine.