
Rais Magufuli (kulia) alipokuwa akiipokea ndege ya Airbus A220 - 300 Dodoma.
Kigwangalla ambaye ni mbunge wa Nzega Vijijini amelazimika kuweka wazi hilo wakati alipokuwa akisifia utendaji kazi wa Rais Magufuli hususani kwenye suala la kununua ndege.
''Unaweza ukasema Kigwangalla Waziri anajikomba, sawa tu! Povu ruksa!'', ni sehemu ya ujumbe wake alioundika kwenye mtandao wa Twitter.
Uthubutu wa Rais Magufuli ni wa dunia nyingine. Utake usitake, umpende umchukie, kazi yake utaikubali tu! Tulihitaji Rais wa aina hii kwa wakati huu, Mungu ametupa! Alhamdulillah . Unaweza ukasema Kigwangalla Waziri anajikomba, sawa tu! Povu ruksa! #TanzaniaUnforgettable pic.twitter.com/fPSwxLQ5RT
— Dr. Kigwangalla, H. (@HKigwangalla) January 10, 2019
Katika Baraza la Mawaziri la kwanza kwenye awamu ya tano chini ya Rais Magufuli, Kigwangalla aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kabla ya kupelekwa kuwa Waziri kamili wa Maliasili na Utalii Oktoba 7, 2017.
Ndege ya pili aina ya Airbus A220-300 iliyopewa jina la Ngorongoro imeondoka nchini Canada jana na inatarajiwa kufika nchini kesho Januari 11, 2018 baada ya kutanguliwa na ile ya kwanza iliyopewa jina la Dodoma ambayo ilitua nchini Desemba 23, 2018.